Msiba huu umetuathiri sana, marehemu ni marafiki na wafanyakazi wenzetu - Joyce Msuya
Masuala ya UM
Wakati maombolezo ya vifo vya wafanyakazi 21 wa Umoja wa Mataifa yakiendelea katika ofisi mbalimbali duniani kote, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP, mjini Nairobi Kenya ni miongoni mwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopata pigo la ajali hiyo.