Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yasema katu haitowasahau mashujaa wa Tanzania waliouawa Semuliki

Mkuu wa operesheni za  ulinzi wa amani Jean-Pierre Lacroix (katikati) alipoitembelea Tanzania kuhani msiba wa walinda amani 15 waliouawa huko DR Congo.
UN Tanzania
Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani Jean-Pierre Lacroix (katikati) alipoitembelea Tanzania kuhani msiba wa walinda amani 15 waliouawa huko DR Congo.

UN yasema katu haitowasahau mashujaa wa Tanzania waliouawa Semuliki

Amani na Usalama

Ikiwa mwezi huu ni umetimu mwaka mmoja tangu walinda amani 15 wa Tanzania wauawe huko Semuliki jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, Umoja wa Mataifa umesema katu hautosahau mchango wao na utaendelea kuenzi kazi yao. 

Visiwani Zanzibar nchini Tanzania, ugeni wa ngazi ya juu kutoka Umoja wa Mataifa ukiongozwa na mkuu wa operesheni za  ulinzi wa amani Jean-Pierre Lacroix na Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DR Congo, Leila Zerrougui.

Lengo kubwa ni kukutana na familia za walinda amani 15 wa Tanzania waliouawa katika shambulio baya katika historia ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa huko DR Congo tarehe 7 mwezi Desemba mwaka jana. Walinda amani hao wa brigedi ya nyuki 101 waliuawa na waasi wa kikundi cha ADF.

Bwana Lacroix na Bi. Zerrougui walikutana na wanafamilia wakiwemo wazazi na wajane na kuzungumza nao kisha mmoja wa Bi. Rosemilya Kamili Degila ambaye ni mama mzazi wa marehemu Deogratius Kamili Rashidi amesema..

Naye Bwana Lacroix akasema.

"Naomba niwahakikishie kwamba, najua ni vigumu kwetu kupata maneno ya kuelezea machungu  yenu, lakini hebu niwahakikishie kuwa kama ambavyo hamuwezi kuwasahau mashujaa wenu jasiri, nasi vivyo hivyo. shambulio hilo Semuliki DRC lilikuwa shambluio baya zaidi dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kwa miongo na miongo."

Hapo jana Bwana Lacroix baada ya kuwasili Tanzania alikuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Augustine Mahiga na tayari amemaliza ziara yake nchini humo.

Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa, tafadhali jisajili na pia unaweza kupakua apu ili kuweza kusikiliza wakati wowote popote ulipo.