Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvua ikianza darasa letu litageuka tope, tusaidieni- Mtoto Asmaa

Familia 400 zimepata hifadhi katika kituo cha makazi ya muda huko Idlib nchini Syria na watoto nao wamepata fursa ya kusomea kwenye mahema
© UNICEF/Aaref Watad

Utamaduni na Elimu

UNICEF inasema zaidi ya watoto milioni 4 nchin Syria wameanza elimu rasmi mwezi uliopita wa Septemba lakini wengine milioni 2 bado hawana fursa ya elimu.

Nchini Syria, mahema yaliyojengwa ili kutoa huduma ya elimu kwa watoto jimboni Idlib yameanza kuleta nuru kwa watoto ambao wamekosa elimu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa kutokana na mapigano kwenye eneo hilo.

Miongoni mwa watoto hao ni Asmaa mwenye umri wa miaka 13 ambaye yey ena familia yake wamekuwa wakilazimika kuhamahama ili kukwepa mapigano jambo ambalo limesababisha akose elimu.

Asmaa ambaye sasa wanaishi kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani huko kaskazini mwa Idlib ana furaha kwa kuwa sasa amerejea darasani kwenye jimbo hilo la Idlib ambako takribani watoto milioni 1 wengi wao wakimbizi wa ndani wamekuwa wakikosa fursa ya elimu.

Mahema sita yaliyojengwa na shirika la Umoja wa Mataifala kuhudumia watoto, UNICEF katika kambi ya muda ya Junaina imetoa fursa kwa watoto 250 wenye umri wa kati ya miaka 7 hadi 14 kupata elimu. Asmaa anafunguka..

(Sauti ya Asmaa)

Shule yetu haina vifaa vingi; vitabu, madaftari na madawati. Hivi sasa tunaketi kwenye chini. Punde majira ya baridi yanawadia. Mvua ikinyesha kila kitu kitakuwa tope. Nataka kujifunza. Tunataka kusoma kwa ajili ya mustakbali wetu. Nataka kuwa mwalimu nifundishe watoto kama mimi na nifanikiwe. ”

Faysal, ambaye ni Mkurugenzi wa shule hii ana furaha kwa kuwa watoto bado wanfika shule wakiwa na furaha na ari ya kusoma ingawa shule haina vifaa vya kutosha.

Shule hii ina walimu 10 wa kujitolea ambao wanajitahidi kwa kadri ya uwezo wao kuelimisha watoto  jambo ambalo limekuwa kichochoe kwa Asmaa kutaka kuwa mwalimu baadaye ili aweze kufindisha watoto wenzake.

UNICEF inasema zaidi ya watoto milioni 4 nchin Syria wameanza elimu rasmi mwezi uliopita wa Septemba lakini wengine milioni 2 bado hawana fursa ya elimu.