Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waathirika wa Ebola DRC wameanza kupewa msaada wa chakula na WFP

WFP yaanzisha mpango wa msaada wa chakula kwa watu walioathirika na Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
WFP/Olivier Nkakudulu
WFP yaanzisha mpango wa msaada wa chakula kwa watu walioathirika na Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Waathirika wa Ebola DRC wameanza kupewa msaada wa chakula na WFP

Afya

Shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula na kilimo dunini WFP limeanza  mpango wa dharura  wa kutoa chakula kwa waathirika wa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Katika taarifa yake iliyotolewa Goma, Mashariki mwa DRC, WFP inasema ikishirikiana na shirika la kimataifa la utoaji misaada la Caritas wanatoa  chakula kwa wagonjwa  na pia watu wengine ambao wamethirika kwa njia moja au nyingine  na mlipuko huo katika maeneo ya Kivu Kaskazini.

Kwa mujibu wa mkuu wa Ofisi ya WFP nchini DRC, Claude Jibir, mlipuko huo wa 10 wa Ebolaumetokea katika eneo ambalo limeghubikwa na vita na watu kutawanywa ambali ambayo inaleta  hatari ya dharura ya kiafya ya kikanda kwa mataifa matatu ya DRC, Rwanda na Uganda.Ameongeza kuwa  kutokana na kuwepo kwa msaada wa chakula, masuala ya kiufundi na kuboreshwa kwa usafiri wa anga  shirika lake  limeazimia kufanya mengi zaidi ili kuokoa maisha ya watu  na kuzuia kuenea kwa mlipuko huo..

WFPhivi sasa ,inapanua wigo wa huduma zake zake na kuwahusisha waathirika wa Ebola  kwani hapo kabla imekuwa ikiwasaidia zaidi  maelfu ya watu walioathirika na vita katika mkoa huo ,na katika kitovu cha mlipuko wa Ebola eneo la Beni, watu 12,000 wasio na makazi  wamekuwa wakisaidiwa na WFP kwa kupewa chakula tangu  mwezi Julai.

Watu takriban 4,000 hupokea  msaada wa chakula  cha kuwatosheleza kwa mwezi mmoja ikiwemo nafaka, maharage, mafuta ya kupikia, na chumvi na kwa wagonjwa wa Ebola wanapewa biskutizinayoongeza nguvu.

Tangu kuzuka kwa mlipuko huo visa 111 vya Ebola vimeorodheshwa  , 83 kuthibitishwa na watu zaidi ya 4,000 wamepewa chanjo.