Maelfu ya watoto wazidi kutoweka DRC

Msichana akiwa amembeba mdogo wake katika mji wa Kalemie, jimbo la Tanganyika,DRC
Picha na UNICEF/Vockel
Msichana akiwa amembeba mdogo wake katika mji wa Kalemie, jimbo la Tanganyika,DRC

Maelfu ya watoto wazidi kutoweka DRC

Haki za binadamu

Maelfu ya watoto wametoweka kusikojulikana katika jimbo la Tanganyika nchini Jamuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, na mama zao wamejotokeza na kupaza sauti wakitaka watoto wao warudishwe.

Kutana na Bi. Augustina Mwamba, mmoja kati ya wanawake waliojitokeza na kudai kuwa  binti yake mwenye umri wa miaka 6 alichukuliwa kusikojulikana kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa….


Sauti ya Augustina

Akiwa ameongozana na wanawake wengine ambao kwa sasa wapo kwenye  kambi ya mpito ya wakimbizi wa ndani nchini humo, Bi Augustina anasema..
 

Sauti ya Augustina

Naye Elizabeth Majuma Ngoy ambaye aliwapoteza binti zake wawili,  kwa uchungu anaelezea zahma iliyowakuta binti zake.
 

Sauti ya Elizabeth Majuma


Hata hivyo kwa Ndiba Kaite yeye ni tofauti kwani watoto wake walirejea nyumbani baada ya kushikiliwa kwa zaidi ya miezi saba. Walirejea kwa msaada wa  mashirika ya kibinadamu ambayo yamekuwa yakijitolea kuzungumza na watekaji nyara .
 

Sauti ya Ndiba Kaite

Wiki hii ofisi ya pamoja ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na DRC ilitoa ripoti yake kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwenye eneo la Kasai.

Vitendo ni pamoja na ubakaji, utekwaji nyara, ukataji wa viungo vya siri na ulaji wa nyama za binadamu.

Umoja wa Mataifa kupitia ofisi hiyo umetoa wito kwa pande zote kinzani kusitisha mara moja mateso dhidi ya raia wasio na hatia na zikae kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tufauti zao.