Mbio za Marathoni zaleta pamoja wakazi wa Goma na Kalemie
Katika kuadhimisha sikukuu ya krismas na mwaka mpya walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO wameshiriki mbio za riadha za nusu marathoni kwenye mji wa Goma, jimbo la Kivu Kaskazini.

Wafanyakazi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakiwa katika mbio za nusu marathoni huko Goma. (Picha:MONUSCO)
Nako huko Kalemie ujumbe wa MUNUSCO uliandaa, michezo na burudani kwa watoto na kutoa zawadi kwa watoto wapatao 250 wenye umri wa kati ya miaka mitano hadi 17, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sikukuu ya krismasi.
Wakati wa sherehe hizo MONUSCO ilitoa dakika kadhaa kuwakumbuka walinda amani waliopoteza uhai wao katika kutimiza majukumu yao ya kulinda raia walio kwenye maaeneo ya mizozo DRC.