Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijiji Afrika kunufaika na umeme rafiki wa mazingira

Mradi wa nishati ya gesi katika kaya moja barani Afrika. Picha: UM/Video capture

Vijiji Afrika kunufaika na umeme rafiki wa mazingira

Jamii za vijijini barani Afrika zitanufaika na nishati endelevu ya umeme baada ya kundi la wawekezaji kuidhinisha nyongeza ya dola milioni 55 kwa ajili ya mradi wa nishati endelevu barani humo. Patrick Newman na taarifa kamili.

(Taarifa ya Patrick Newman)

Tovuti ya ClimateAction inayochapisha taarifa kuhusu hatua zinazochukuliwa kufanikisha nishati isiyoharibu mazingira imesema mradi huo unatekelezwa wakati ambapo takwimu zinaonesha kuwa karibu watu milioni 600 katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Shara hawana nishati ya umeme.

Dola milioni 30 zimetolewa na Benki ya Maendeleo Afrika ADB, ambapo kampuni za giridi ya umeme zitapatiwa mikopo ili zisaidie kaya vijijini kupata umeme usioathiri mazingira.

Wawekezaji wengine katika mradi huo ni kampuni iitwayo Calvert Impact Capital iliyotoa dola milioni 10, huku fuko la mazingra dunianik, likichangia  dola milioni 8.5 na mfuko wa maendeleo wan chi za Nordic ukitoa dola milioni 6.5

Mradi huo we umeme vijijini unatarajia kupunguza tani milioni nane za hewa ukaa ambapo kaya milioni 75 zitakuwa zimepata  nishati hiyo inayolinda mazingira ifikapo mwaka 2025.