Watoto milioni 3 wanazaliwa vitani Yemen kila mwaka:UNICEF

16 Januari 2018

Watoto zaidi ya milioni tatu wamezaliwa nchini Yemen tangu kuanza kwa machafuko mwezi Machi 2015 kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na shirika la Kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF. Sitaj Kalyango na tarifa kamili

(TAARIFA YA SIRAJ KALYYANGO)

Ripoti hiyo iitwayo “Kuzaliwa vitani” inafafanua jinsi gani watoto nchini Yemeni wameaachwa na makovu ya miaka ya machafuko, kutawanywa, maradhi, umasikini, utapia mlo na ukosefu wa huduma za msingi kama maji, afya na elimu.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa UNICEF nchini Yemen Merixtell Relanyo kizazo chote cha watoto nchini Yemen kinakuwa kwa kutojua lolote isipokuwa vita na machafuko.

Watoto hao wanakabiliwa na athari kubwa za vita ambavyo hawavijui chanzo chake, huku utapia mlo na maradhi vikiongezeka kutokana na kusambaratika kwa mfumo wa afya. Bi relano ameongeza kuwa

(SAUTI YA RELANO)

“Watoto 25,000 wanafariki dunia wakati wa kuzaliwa kila mwaka au mwezi wa kwanza wa Maisha yao , kwa sababu wengi wao huzaliwa nje ya hospitali hivyo bila kuwepo na wakunga wenye ujuzi , na hivyo kuwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa maradhi na vifo.”

Ameongeza kuwa hata wanaonusurika kifo wengi husalia na vilema vya maisha vya kimwili na kisaikolojia

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud