Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madhila dhidi ya raia yaongezeka mzozoni Ukraine; UM

Waathirka wa vita vinavyoendelea Ukraine Mashariki. Picha: IOM/UN/Volodymyr Shuvayev

Madhila dhidi ya raia yaongezeka mzozoni Ukraine; UM

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo inasema madhila dhidi ya raia katika mzozo wa kivita nchini Ukraine huenda yakaongezeka zaidi, kufuatia kuibika upya kwa mapigano.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo inasema madhila dhidi ya raia katika mzozo wa kivita nchini Ukraine huenda yakaongezeka zaidi, kufuatia kuibika upya kwa mapigano.

Ripoti hiyo inasema mapigano hayo yameathiri watu milioni nne nukta nne kwa sasa, yakisababisha vifo zaidi na uharibifu mpya kwa miundombinu muhimu ya maji inayohifadhi kemikali hatari, kinachotishia uhai wa binadamu na mazingira.

Haya yote yakitokana na ukiukwaji wa mara kadhaa wa mikataba ya kusitisha mapigano.

Fiona Frazer, Mkuu wa Ujumbe wa Mataifa wa Ufuatiliaji wa Haki za Biandamu, Ukraine, amesema mmoja wa raia aliwaeleza wafanyakazi wa ujumbe huo, kwamba hali imechafuka zaidi ikilinganishwa na mwaka 2014, kiasi kwamba haivumiliwi kwa sasa.

Ujumbe huo ulisajili vifo vya raia 15 vinavyohusiana na mzozo huo, na visa vingine 72 vya waliojeruhiwa kati ya Agosti 16 na  Novemba, 15 mwaka huu.