Kuondoka kwa kaka, familia imepoteza dira- Yasir

12 Disemba 2017

Nchini Tanzania uchunguzi wa miili ya walinda amani waliouawa kwenye shambulizi huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC unaendelea wakati huu ambapo wafiwa nao wamezungumzia vile ambavyo wamepokea msiba huo.

Kwa mujibu wa afisa wa habari wa kituo cha habari za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, UNIC, Stella Vuzo, uchunguzi wa miili hiyo 14 unafanyika jijini Dar es salaam huku ikielezwa kuwa walinda amani 12 wanatoka Zanzibar ilhali mmoja anatoka Tanga na mwingine Iringa.

Amesema ni kutokana na hilo, hadi sasa ndugu na jamaa bado hawajaweza kuona miili ya ndugu zao na kwamba shughuli za kuona miili hiyo itafanyika kesho Jumatano jijini Dar es salaam na kufuatia na ibada rasmi ya serikali ya kuaga miili siku ya Alhamisi

Miongoni mwa waliopoteza ndugu zao ni Bwana Yasir Ali Hamadi kutoka Zanzibar ambaye akizungumza na Bi. Vuzo amesema mmoja wa walinda amani hao ni kaka yake ambaye pia alikuwa ni tegemo la familia.

(Sauti ya Yasir Ali Hamadi)

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter