Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumejizatiti kuendelea na ulinzi wa amani wa UM- Tanzania

Walinda amani wa Tanzania kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, (FIB) cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko DRC, MONUSCO. (Picha:MONUSCO/Force)

Tumejizatiti kuendelea na ulinzi wa amani wa UM- Tanzania

Tanzania imesema ni matumaini yake kuwa mkutano wa mawaziri wa ulinzi huko Vancouver Canada utafungua njia zaidi ya kuboresha operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa.

Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano huo, Waziri wa Tanzania wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  Dkt. Hussein Mwinyi amegusia masuala ya marekebisho ya operesheni hizo akisema..

(Sauti ya Dkt. Mwinyi)

Alipoulizwa iwapo Tanzania iko tayari kuendelea na operesheni hizo za ulinzi wa amani, Dkt. Mwinyi amesema..

(Sauti ya Dkt. Mwinyi)

Kwa mujibu wa Dkt. Mwinyi, Tanzania itapeleka vikosi vyake pia huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini.

Mkutano huo wa siku mbili umeanza jana jumanne na umeleta pamoja wawakilishi na mawaziri kutoka nchi 80 wanachama wa Umoja wa Mataifa.