Vitisho dhidi ya wataalamu wa haki za binadamu vikome Burundi:UM

21 Novemba 2017

Serikali ya Burundi kupitia mwakilishi wake wa kudumu  katika Umoja wa mataifa imetupilia mbali tuhuma za vitisho na  ukiukwaji wa haki za binadamu katika mkutano wa tume la haki za binadamu wa kujadili mustakabali wa nchini hiyo na  wawakilishi 47, pamoja jopo la watalum wa haki za binadamu. John Kibego na taarifa kamili

(TAARIFA YA JOHN KIBEGO)

Kupitia taarifa ya msemaji wa ofisi ya haki za binadamu mjini Geneva Uswis Rupert Colville , Kamishna Mkuu  wa  haki za binadamu ameiambia Serikali ya Burundi  kuwa tume ya haki za binadamu  haiwezi kutiliwa mashaka kuhusu maamuzi yake, kwani imefanya uchunguzi kwa kuzingatia kanuni ilizowekewa na  bazara la usalma  na hivyo

(SAUTI YA COLVILLE)

“Vitisho vya Serikali ya Burundi kutokubali maamuzi ya tume  ni ukiukwaji wa wazi wa kifungu cha VI cha mkataba wa mwaka 1946 kuhusu haki na kinga ya Umoja wa Mataifa .

Pia ia amesisitiza kwamba ni lazima serikali ya Burundi irekebishe sera zake za kukataa kushirikiana na tume ya Kimataifa ya uchunguzi wa wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo na iache mara moja kutishia wanachama wake.

Kamishna Mkuu pia emekemea vitisho vya mara kwa mara dhidi ya watalam wa haki za binadamu  wa Umoja wa Mataifa  na wanaharakati wengine wa kupigania haki za binadamu nchini humo.