Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ibara kwa Ibara- Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa

Ibara kwa Ibara- Tamko la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi disemba mwaka 2018 linatimiza miaka 70. Tamko hilo ni msingi wa haki za binadamu ulimwenguni na lilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1948. Kwa kutambua umuhimu wake, ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inaanza kampeni ya kulipigia chepuo. Nasi kwenye Idhaa ya Kiswahili tunakuletea ibara za tamko hilo. Ibara ziko 30 nasi tunakuletea ibara moja kila siku. Hii leo tunakuletea Ibara ya kwanza na Selina Jerobon.

Ibara ya 1: Watu wote wamezaliwa huru, hadhi na haki zao ni sawa. Wote wamejaliwa akili na dhamiri, hivyo yapasa watendeane kindugu.