Msaada wa kimataifa ni nyota ya jaha baada ya shambulio Somalia

19 Oktoba 2017

Raia wa Somalia wameandamana katika mitaa yam ji mkuu Moghadishu kupinga ukatili wa itikadi kali baada ya shambulio kubwa kabisa la bomu kuwahi kutokea nchini humo na kukatili Maisha ya watu zaidi ya 300 mwisho wa wiki iliyopita.

Umoja wa Mataifa na washirika wake wamekuwa wakiisaidia serikali kukabiliana na athari na mahitaji makubwa yaliyosababishwa na shambulio hilo.

Naibu mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini  Somalia Vincent Lelei, amesema msaada wa jumuiya ya kimataifa kwa Somalia baada ya shambulio hilo ni kama nyota ya jaha na msaada wa kwanza walioutoa ni

(CUT LELEI)

“Mashine kubwa za kuondoa mabaki mazito ya vifusi ambayo inawezekana yalikuwa yanawakandamiza watu ambao pengine wako hai, kuondoa kifusi, kusafisha eneo hilo , kuondoa maiti , kuokoa maisha ya watu waliokuwa bado hai, kudumisha usalama wa neo hilo na kurejesha utulivu.”

Amesema hata hivyo Somalia imeshuhudia ukaribu wa Ulimwengu baada ya zahma hiyo

(LELEI CUT 2)

“Kumekuwa na mwitio mkubwa sana wa zahma hii nchi mbalimbali wanachama wameleta msaada na wataalamu kama Uturuki, Uingereza, Marekani, Kenya , Qatar, Djobouti, makampuni mbalimbali ya Somalia, mashirika ya Umoja wa Mataifa , imekuwa ni masikitiko kwa kila mtu , lakini pia imekuwa ni kama nyota ya jaha iliyowateta wadau wote na nchi waanchama kushirikiana kwa pamoja “