Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya mtoto wa kike duniani yaadhimishwa leo

Siku ya mtoto wa kike duniani yaadhimishwa leo

Leo ni siku ya mtoto wa Kike duniani ambapo ujumbe unajikita kwenye kuwezesha mtoto wa kike kabla, wakati na baada ya majanga, matukio mbali mbali yakifanyika ulimwenguni kuangazia siku hii adhimu. Selina Jerobon na taarifa kamili.

(Taarifa ya Selina)

Nats..

Kibao hicho cha Kate Perry, balozi mwema wa shirika la la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika video mahsusi akipazia sauti umuhimu wa hatua bora ili kumwezesha mtoto wa Kike wa leo awe bingwa siku za usoni.

Na kwa mwaka huu Umoja wa Mataifa unatumia ujumbe wake kuangazia watoto wa kike bilioni 1.1   kote duniani ambao ni chanzo cha ari, ubunifu na uthabiti, ukitaka walindwe na wawekewe mazingira bora ili kumaliza ukatili dhidi yao.

Hata hivyo nchini Uganda, watoto wenyewe wa Kike wamechukua hatua kujilinda dhidi ya ukatili kama anavyoelezea Khadija Agondwa.

image
Msichana Khadijah Agondwa wa wilayani Buliisa nchini Uganda akieleza jinsi anavyoilinda dhidi ya ukatili. (picha:Idhaa ya Kiswahili/John Kibego)
(Sauti ya Khadija)

Na nchini Tanzania, Rebeca Gyumi ambaye ni mshindi wa tuzo ya UNICEF na pia muasisi na mwenyekiti wa Msichana Initiative anasema mafanikio yaliyopatikana hadi sasa katika harakati za kumlinda mtoto wa kike..

(Sauti ya Rebecca)