Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalam wa haki za binadamu ziarani Guyana kuchunguza ubaguzi

Wataalam wa haki za binadamu ziarani Guyana kuchunguza ubaguzi

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wenye asili ya  kiafrika  watatembelea kisiwa cha Guyaha kuanzia tarehe 2 hadi 9 mwezi ujao wa Oktoba ikiwa ni hatua ya kujifunza hali ya haki za binadamu kwa watu wenye asili ya  Afrika waishio katika visiwa hivyo.

Msemaji wa msafara huo Sabelo Gumeze amesema wakati wa ziara hiyo watakusanya taarifa zozoe kuhusiana na ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kiitikadi na pia ripoti yoyote inayolenga chuki, ili waifanyie tathmini ya ukiukwaji wa haki ya binadamu kundi hilo.

Wataalamu hao watatumia ziara yao kuendelza kampeni  ya muongo ya kimataifa wa watu wenye asili  wa kiafrika uliotangazwa mwaka 2015 hadi 2024, yenye lengo la kupongeza  michango mbalimbali ya watu wenye asili ya kiafrika kwa jamii.

Halikadhalika kuimarisha ushirikiano wa kitaifa, kikanda na kimataifa ili kuhakikisha haki za binadamu za watu wa Afrika wanaheshimiwa, kulindwa  duniani kote.

Wataalamu wengine ni Michal Balcerzak na Ahmed Reid ambapo wakiwa huko Guyana watakuwa na mazungumzo na viongozi wa kiserikali, jamii husika, mashirika ya kiraia na  pia wanaharakati wa masuala ya ubaguzi wa rangi .