Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani yahitaji diplomasia na si vitisho- Tanzania

Amani yahitaji diplomasia na si vitisho- Tanzania

Tanzania imesema itatumia hotuba yake kwenye mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumamosi kutanabaisha masuala kadhaa ikiwemo umuhimu wa diplomasia katika kutatua mzozo hususan ule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK ikijulikana pia Korea Kaskazini.

Waziri wa Tanzania wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga amesema hayo alipohojiwa na idhaa hii jijini New York, Marekani akisema kuwa hatua hiyo inatokana na vitisho vilivyotolewa na baadhi ya nchi dhidi ya taifa hilo.

(Sauti ya Balozi Mahiga)

Akizungumzia azimio lililowasilishwa na Marekani wiki hii kuhusu marekebisho ya Umoja wa Mataifa, Balozi Mahiga amesema ajenda hiyo muhimu imekuwepo kwa miongo mitatu sasa na haijakabiliwa na upinzani…

(Sauti ya Balozi Mahiga)

Hotuba ya Jumamosi ya Waziri Mahiga itaonyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni ya mtandaoni ya Umoja wa Mataifa http://webtv.un.org/