Baada ya miaka Mitatu msaafara wa misaada wa UNHCR wawasili Deir Ez-Zor
Msafara wa kwanza wa misaada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, umewasili katika mji wa Deir Ez-Zor uliopo mashariki mwa Syria, baada ya miaka mitatau.
UNHCR inasema , malori matano ya misaada yaliwasili Deir Ez-Zor jana Septemba 14 baada ya safari ya saa 22 kutoka kwenye ghala la UNHCR huko Homs. Msafara huo ulibeba vifaa muhimu vya kujikimu vya ujenzi, mahema, taa zitumiazo mwanga wa jua, vifaa vya jikoni na usafi vinavyokadiriwa kuwahudumia watu 30,000.
Halikadhalika kuna watu 93,000 huko Deir Ez-Zor ambalo ni jiji kubwa zaidi mashariki mwa Syria linalozingirwa na waasi tangu na 2014. Msaada wa awali umepelekwa kwa njia ya anga na WFP , kabla ya ngome ya waasi kubomolewa na kuruhusu mashirika ya misaada kuwafikia anagalau watu 75000 amabo ni wahitaji wa misaada ya kibinaadamu huko Deir Ez-Zor.
Kutokana na hali ya kiusalama kutoka miji ya Deir Ez-Zor na Ar-Raqqa UNHCR inasisitiza wito wake wa kulinda walioko kwenye maeneo ya mgogoro na kuzitaka pande husika kuheshimu kanuni za kimataifa za kibinadamu. Zaidi ya raia wa Syria milioni 4.5 bado wapo kwenye maeneo yenye migogoro na yasiyofikika .