Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres alaani jaribio lingine la kombora kutoka DPRK

Guterres alaani jaribio lingine la kombora kutoka DPRK

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali jaribio lingine la nyuklia lililofanywa leo na Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake imemnukuu Katibu Mkuu akisema kwamba jaribio hilo ambalo linakiuka azimio la Baraza la Usalama limekuja siku chache baada ya jaribio la sita la nyuklia lililofanywa na DPRK.

Guterres ametoa wito kwa mamlaka ya DPRK kusitisha mara moja majaribio hayo,  kuzingatia maazimio ya Baraza la Usalama na kufungua milango ili mazungumzo kuhusu suala hilo yaweze kufanyika.

Katibu huyo atakuwa na mazungumzo kuhusu hali ya rasi ya Korea na wadau wakati wa mjadala wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wiki ijayo.