Neno la wiki - Matamata

Neno la wiki - Matamata

Wiki hii tunaangazia neno "Matamata" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema neno "Matamata" ni hali ya kupepesuka aliyo nayo mtoto anayejifunza kutembea, ama mtu mzima ambaye ni mgonjwa na anajipa mazoezi ya kutembea polepole.  Ameongeza kuwa neno hili haina uhusiano na na neno "kujikongoja".