Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Doria za usiku kufanyika Torit, Sudan Kusini- UNMISS

Doria za usiku kufanyika Torit, Sudan Kusini- UNMISS

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini , UNMISS umepanga kuimarisha doria yake kwenye mji wa Torit kwenye jimbo la Imatong ili kuweka fursa nzuri ya ustawi na maendeleo.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, David Shearer amesema hayo baada ya mazungumzo na gavana wa jimbo  hilo akisema kuwa doria hizo zitahusisha doria za askari wa miguu usiku kucha ili kuweka mazingira salama.

(Sauti ya Shearer)

“Tunaamini kuwa Torit ina fursa nyingi sana. Ina watu wachapakazi na ina udongo mzuri. Inapaswa kuwa moja ya maeneo yenye ustawi zaidi kwenye nchi hii. Nadhani tuko katika mwelekeo bora wa kuweka mustakhbali huo.”

Bwana Shearer ambaye pia ni Mkuu wa UNMISS amesema doria hizo ni mwendelezo na kwamba amemweleza Gavana wa Imatong kuwa ..

(Sauti ya Shearer)

“Watu wetu wa UNMISS ambao wamekuwa wanafanya doria, nadhani wameweka pengine mazingira bora ya utulivu na kujiamini. Nimeeleza zaidi kuwa ni kwa muktadha huo ndio maana wameweza kufanya hivyo.”

Tayari Umoja wa Mataifa uliridhia kupelekwa kwa jeshi la kikanda nchini Sudan Kusini na uwepo wao utawezesha kupanuka kwa shughuli za doria hadi kwenye mji kama Torit na hivyo kuweka mazingira salama ya usafiri na biashara.