Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shida haibagui wala haichagui, tusaidiane: Mugenyi

Shida haibagui wala haichagui, tusaidiane: Mugenyi

Shida haina adabu, haichagui , wala haibagui inapokufika imekufika, la msingi kusaidiana. Huo ni wito wa Iddi Mugenyi mkurugenzi wa shule ya sekondari ya East african Muslim High school iliyoko nchini Uganda. Shuleni kwake anasaidia watoto wakimbizi takribani 50 hususan masuala ya karo ili waweze kupata elimu ambayo ni ufunguo wa maisha. Anawaasa Waganda wenzie na dunia kwa ujumla kwamba ni vyema kuwasaidia wahitaji kwani sote ni binadamu na leo kwao kesho kwetu. Ameketi na mwandishi wetu wa Uganda John Kibego na kujadili umuhimu wa misaada ya kibinadamu kwa wanaokumbwa na matatizo.