Neno la wiki: Sogi

18 Agosti 2017

Wiki hii tunaangazia neno “Sogi” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.

Bwana Sigalla anasema Sogi ni mifuko miwili anayebebeshwa punda, moja kila upande ambayo hutumiwa kubeba mizigo ndani yake.