Watoto zaidi ya 100 wapoteza Maisha kwenye maporomoko ya udongo Sierra Leon- UNICEF

17 Agosti 2017

Timu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ipo nchini Sierra leon ili kutoa msaada wa dharura kwa familia zilizoathirika na maporomoko ya udongo na mafuriko mjini Freetown . Grace Kaneiya na tarifa zaidi

(TAARIFA YA GRACE)

Shirika hilo linasema mamia ya watu wamepoteza maisha wakiwemo watoto 109 na idadi inatarajiwa kuongezeka kwa sababu watu zaidi ya 600 wakiwemo watoto bado hawajulikani waliko.

UNICEF inasema uharibifu ni mkubwa na maelfu ya watoto wameachwa bila makazi, wakiwa katika hali mbaya na bila msaada hivyo imetoa wito wa kuhakikisha watoto hao wanalindwa dhidi ya maradhi na unyanyasaji.

Tangu Jumatatu ilipozuka zahma hiyo UNICEF imekuwa ikigawa msaada yakiwemo maji safi ya kunywa, vifaa vya kujisafi, dawa, mahema na msaada wa ushauri nasaha.