Vijana kushirikiana katika kufanikisha SDGs: Tanzania

16 Agosti 2017

Umoja wa Mataifa unapigia chepuo vijana kuwa bega kwa bega katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, hususan lile la kwanza la kutokomeza umaskini bila kusahau usawa wa kijinsia. Na ni kwa mantiki hiyo shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UNWomen nchini Tanzania mwaka 2015 lilizindua programu ya maendeleo endelevu kupitia ujasiriamali, ikilenga vijana wa kike walio maeneo ya mipakani na nchi hiyo. Tayari matunda yameanza kuonekana hivi sasa na si tu kwa vijana wa kike bali kwa jamii ile inayowazunguka na safari ndio imeanza kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.