Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterress alaani mfululizo wa mashambulizi Nigeria

Guterress alaani mfululizo wa mashambulizi Nigeria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika Agosti 15 katika jimbo la Borno nchini Nigeria.

Kupitia msemaji wake, ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Nigeria kufuatia vifo na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Katibu Mkuu pia ametoa wito waliotekeleza uhalifu huo nchini Nigeria na nchi jirani wafikishwe katika vyombo vya sheria.

Wakati huohuo Guterres amesisitiza mshikamano wa Umoja wa Mataifa na serikali ya Nigeria katika vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali.

Aidha ameelezea dhamira ya Umoja huo kusaidia katika juhudi zilizo chini ya mkataba wa kupinga ugaidi za kamisheni ya ziwa Chad.