Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres astushwa na vifo vya maporomoko ya udogo na mafuriko Sierra Leone:

Guterres astushwa na vifo vya maporomoko ya udogo na mafuriko Sierra Leone:

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na vifo na athari zilizosababishwa na maporomoko ya udongo na mafuriko kwenye miji ya Regent na mji mkuu Freetown nchini Sierra Leone.

Kupitia tarifa ya msemaji wake Guterres, ametuma salamu za rambirambi kwa watu na serikali ya Sierra Leone kufuatia vifo hivyo na uharibifu uliosababishwa na janga hilo la asili.

Duru zinasema takribani watu 200 wamepoteza Maisha kutokana na maporomoko na mafuriko hayo. Katibu Mkuu amesema anashikamana na watu na serikali ya Sierra Leone na kwamba Umoja wa Mataifa uko pamoja nao katika juhudi za uokozi zinazoendelea.