Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwepo wa UM jimboni Darfur umebadili maisha yetu- mkazi Darfur

Uwepo wa UM jimboni Darfur umebadili maisha yetu- mkazi Darfur

Wakati siku ya utu wa kibinadamu ikiadhimishwa tarehe 19 mwezi huu, wakazi jimboni Darfur nchini Sudan wameupongeza Umoja wa Mataifa kwa huduma wanazozipata kupitia Umoja huo.Taarifa kamili na Luteni Selemani Semunyu wa radio ya Umoja wa Mataida Darfur UNAMID

(TAARIFA YA SELEMANI)

Hii ni kufuatia ujio wa wawakilishi kutoka Mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la kuhudumia watoto UNICEF kwenye vijiji vya Mershing na Almalam jimboni Darfuru nchini humo.

Akina mama na vijana ni miongoni mwa wanufaika wa huduma hizo na nimekutana nao katika pilka pilka zangu kwenye kituo cha Mershing ambacho kilitembelewa na wawakilishi kutoka UNICEF.

Kwanza kabisa nimekutana na Shezah Adam, mkazi wa Mershing ambaye anasema maisha yao yamebadilika kufuatia uwepo wa Umoja wa Mataifa na huduma ambazo ziliwagharimu pesa hapo awali sasa wanazipata bila ya malipo..

(Sauti ya Shezah)

"Kwa kawaida tunakutana mara moja kwa wiki na wanatupa mafunzo na kwa mtazamo wangu walinda amani wa UNAMID wana uhusiano mzuri na jamii."

Kwa upande wake mkuuu wa kituo cha Mershing Abdallah Haroun Mohameda akielezea shukrani zake ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuendelea kutoa huduma hususan katika kukabiliana na shida za maji, moja ya huduma ilioathiri kaya nyingi katika vijiji hivyo.

(Sauti ya Abdallah)

"Kituo hiki sio tu kinatoa huduma kwa watoto lakini pia kwa wanawake, lakini kama unayoona kinahitaji ukarabati, kwani majengo ni makuukuu na yanahitaji kukarabatiwa upya."