Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tulindeni ili tuweze kutoa huduma za kiutu #NotaTarget - Hussein

Tulindeni ili tuweze kutoa huduma za kiutu #NotaTarget - Hussein

Kuelekea siku ya utu wa kibinadamu tarehe 19 mwezi huu, wakimbizi ambao wanatumika kutoa huduma za kijamii kwenye kambi ya Daadab nchini Kenya wamesema ukosefu wa usalama unakwamisha huduma zao.

Hussein Issack mkimbizi kutoka Somalia ambaye hivi sasa ni mwalimu mkuu wa shule ya Gateway kambini hapo amesema wana uhaba wa vifaa vya kufundishia na hata pale watoa misaada wanataka kuwasilisha vifaa wanakumbwa na changamoto, akisema wahudumu hao..

(Sauti ya Hussein)

Hata hivyo Hussein ambaye anafundisha Biolojia na Historia wakiwa chini ya shirika lisilo la kiserikali la Refugee Education Trust, RET, amesema licha ya changamoto ya usalama bado wafanyakazi hao wanaweza kujitoa kwa hali na mali kwa kuwa..

(Sauti ya Hussein)