Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunafuatilia kwa karibu hali nchini Kenya-UM

Tunafuatilia kwa karibu hali nchini Kenya-UM

Umoja wa Mataifa umesema unafuatilia kwa karibu hali nchini Kenya, wakati huu ambapo matokea ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8 yanatarajiwa kutangazwa.

Akizungumza na waaandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini New York, Marekani, msemaji wa katibu mkuu Stéphane Dujarric amesema Umoja wa Mataifa haukuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi lakini..

(Sauti ya Stéphane Dujarric)

“Nadhani kilicho muhimu ni kwamba wadau wote, na watu wa Kenya waruhusu mchakato ufanyike, na iwapo wana malalamiko wayaelekeze kupitia vyombo vya sheria na kwa njia ya amani.”

Umoja wa Mataifa kupitia taarifa ya msemaji huyo umesisitiza wito wa Katibu Mkuu wa kuzingatia hali ya utulivu na kuheshimu haki za binadamu na uhuru hususan wakati huu watu wakisubiri kwa hamu matokeo rasmi.