Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia bado inasuasua na haki za watu wa asili miaka 10 baada ya azimio:

Dunia bado inasuasua na haki za watu wa asili miaka 10 baada ya azimio:

Watu wa asili duniani bado wanakabiliwa na changamoto kubwa muongo mmoja baada ya azimio la kihistoria kuhusu haki za watu wa asili kupitishwa na baraza kuu limeonya leo kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Wakizungumza kabla ya siku ya watu wa asili duniani ambayo hufanyika kila mwaka Agosti 9 , kundi hilo la wataalamu wa haki za binadamu limesema nchi ni lazima zigeuze maneno kuwa vitendo ili kukomesha ubaguzi, kutengwa na ukosefu wa ulizi vikishajihishwa na vitendo vibaya vya mauaji ya watetezi wa haki za binadamu.

Katika taarifa ya pamoja mwenyekiti wa jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili, mtaalamu wa mkakati wa Umoja wa Mataifa wa watu wa asili na mwakilishi maalumu wa haki za watu wa asili wamesema miaka 10 tangu kupitishwa kwa azimio hilo ambalo ni muongozo wa utekelezaji wa haki za watu wa asili bado kuna changamoto,na sasa watu wa asili wanakabiliwa na mtihani mkubwa na ukiukwaji wa haki zao kuliko hata ilivyokuwa miaka 10 iliyopita.

Wameongeza kuwa watu hao wanabaguliwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo afya, elimu, jinsia,ajira, wanapokonywa ardhi zao na kutoshirikishwa katika maamuzi.