Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM kufunguliwa Liberia 2018

Ofisi ya haki za binadamu ya UM kufunguliwa Liberia 2018

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu haki za binadamu Andrew Gilmour leo amehitimisha ziara ya siku tatu nchini Liberia.

Lengo la zira yake ilikuwa ni kuanzisha ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini humo , na mkataba umetiwa saini na serikali kukubali kuanzishwa ofisi hiyo mpya mapema mwaka 2018.

Mwisho wa ziara yake Bwana Gilmour amesema Liberia imepiga hatua kubwa tangu alipozuru mara ya mwisho mara baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe .

Amesema hatua hiyo ni pongezi kwa watu na serikali ya Liberia na kwa juhudi kubwa za mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMIL, hata hivyo amesema masuala ya haki za binadamu bado ni changamoto na yanahitaji kuendelea kwa msaada wa Umoja wa Mataifa.

Akiwa nchini humo alikutana na Rais wa Liberia , mawaziri mbalimbali, viongozi wa asasi za kiraia na mabalozi mbalimbali. Gilmour pia ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuendelea kwa vitendo vya ukeketaji nchini humo na kuitaka serikali kuongeza juhudi kuchagiza kukomeshwa kwa vitendo hivyo.