Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhaba wa maziwa na athari zake mkoani Kagera Tanzania

Uhaba wa maziwa na athari zake mkoani Kagera Tanzania

Shirika la afya ulimwenguni WHO, linasema maziwa ni miongoni mwa lishe muhimu hususani kwa ukuaji wa mtoto na afya ya mwanadamu. Kukosa maziwa hasa kwa watoto wa umri wa miaka mitano ni kukosa lishe muhimu na lishe duni huchangia vifo milioni 2.7 vya watoto kwa mwaka sawa na asilimia 45 ya watoto kote duniani.

Binadamu anapaswa kunywa takribani lita 200 za maziwa kwa mwaka , lakini kutokana na sababu mbalimbali, zikiwemo za kiuchumi, kimazingira na umasikini vimewafanya watu wengi kushindwa kupata lishe hiyo muhimu. Mkoa wa Kagera nchini Tanzania ni moja ya sehemu zinazokabiliwa na uhaba wa maziwa kama alivyobaini Nicholaus Ngaiza wa redio washirika Kasbante FM ya mkoani humo