Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP, IOM na serikali kusaidia waathirika wa ukame Somalia

UNDP, IOM na serikali kusaidia waathirika wa ukame Somalia

Baada ya ukame mkali uliowatawanya na kuwaathiri watu zaidi ya laki nane nchini Somalia , sasa serikali ya nchi hiyo imeshikamana na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM na shirika la Umoja wa Mataifa la mpangomwa maendeleo UNDP ili kuboresha juhudi na uwezo wa kukabiliana na ukame.

Washirika hao watatu wameandaa mafunzo ya siku nne ya kujenga uwezo wa kukabiliana na watu waliotawanywa yakijikita katika uratibu na usimamizi hasa kwenye makambi na juhudi za mwanzo za kujikwamua.

Washiriki zaidi ya 30 wanahudhuria mafunzo hayo zikiwemo wizara za serikali, mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali na Umoja wa Mataifa. Lengo kuu ni kusaidia kuwa na mikakati thabiti ya kukabiliana na dharura pamoja na kusaidia juhudi za serikali za mipango imara ya kudhibiti vyema majanga.