Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suala la uzazi wa mpango nchini Uganda

Suala la uzazi wa mpango nchini Uganda

[caption id="attachment_323712" align="aligncenter" width="625"]02MakalauzaziwampangoUganda

Suala la uzazi wa mpango ni changamoto hususani kwa mataifa yanayoendelea na hususan  Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA takribani wanawake milioni 225 kote duniani ambao wanataka kuepuka mimba zisizotarajiwa hawatumii njia salama na muafaka za kupanga uzazi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukosa taarifa, kutoungwa mkono na wenzi wao au jamii na imani potofu huku asilimia kubwa ya wanawake hao wako katika nchi 69 masikini duniani hasa barani Afrika.

Sasa Umoja wa Mataigfa unahimiza ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu hapo 2030 suala la uzazi wa mpango lazima lipewe kipaumbele. Uganda ni moja ya nchi za Afrika ambazo zimetajwa kuwa idadi ya watu inaongezeka kwa kasi, je suala la uzazi wa mpango kwa wakazi wa nchi hiyo wanalichukuliaje? Ungana na mwandishi wetu John Kibego