Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wahofia ghasia zaidi Venezuela

UM wahofia ghasia zaidi Venezuela

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa leo imesema inahofia ghasia zaidi nchini Venezuela, ambako uchaguzi wa bunge ulioitishwa na rais Nicolas Maduro unatarajiwa kufanyika Jumapili.

Matakwa ya watu wa Venezuela kushiriki katika uchaguzi huo ama la ni lazima yaheshimiwe imesema ofisi hiyo, na kuongeza kuwa mtu yeyote asishinikizwe kupiga kura huku walio tayari kushiriki basi waruhusiwe kufanya hivyo.

(Suti ya  Liz Throssell)

“Tunaitaka serikali kudhibiti maandamano yoyote dhidi ya uchaguzi wa bunge kwa kuzingatia sheria na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu , na hivyo tunahofia kwamba maandamano ambayo utawala unayaona kama yanavuruga uchaguzi yamepigwa marufuku kuanzia leo hadi Agost Mosi. Pia tunatoa wito kwa wale wanaopinga uchaguzi na wanaokusanyika kufanya hivyo kwa amani.”