Hofu yaongezeka machafuko yakishika kasi CAR-UNHCR

30 Juni 2017

Kuzuka upya kwa machafuko yanayoshuhudiwa katika baadhi ya sehemu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kunalitia hofu shirika la Umoja wa Mastaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Machafuko hayo mapya baina ya makundi ya ulinzi na makundi mengine yenye silaha yanaendelea katika miji ya Zemio, Bria na Kaga Bandaro Kusini na Kaskazini mwa CAR huku raia na wafanyakazi wa misaada wakilengwa. Andrej Mahecic ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA MAHECIC)

“Zemio baadhi ya nyumba kar ibu na ofisi ya UNHCR zimechomwa moto, watu zaidi ya 1000 wamekimbia nyumba zao wengi wakipata hifadhi katika kanisa Katoliki mjini humo, wakati wengine 66 wametafuta usalama katika majengo ya UNHCR miongoni mwao wanawake na watoto wanaohofia maisha yao.

Vita CAR vimewafanya watu zaidi ya 500,000 kuwa wakimbizi wa ndani na zaidi ya laki nne kutafutahifadhi nchi jirani za Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Chad na Congo Brazaville.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter