Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwa miaka 13 machafuko na ukwepaji sheria vimetawala CAR:UM

Kwa miaka 13 machafuko na ukwepaji sheria vimetawala CAR:UM

Mauaji na ukiukaji mwingine mkubwa wa haki za binadamu vimeorodheshwa katika ripoti ya Umoja wa Mataifa inayogusia machafuko kadhaa yaliyojiri Jamhuri ya Afrika ya Kati , CAR mwaka 2003 hadi 2015. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Ripoti hiyo iliyotolewa Jumanne na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa na mpango wa Umoja wa Mataifa CAR, MINUSCA, inasema asilimia kubwa ya ukiukwaji huo unaweza kuwa ni uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu huku ikiainisha mkakati wa kukabiliana na ukwepaji sheria uliotawala nchini CAR. Msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ni Ravina Shamdasani anafafanua kuhusu vitendo hivyo

(SAUTI YA RAVINA)

“Ripoti inaorodhesha matukio 620 ikiwemo vitendo vya kutisha vya uchomaji kabisa wa vijiji na mashambulizi ya kulipiza kisasi, ubakaji wa wanawake na wasicha wengine wadogo kabisa wa miaka 5 ambao unaofanywa na makundi ya uhalifu”

Ameongeza kuwa vitendo vingine ni mauaji ya kutumia nguvu kufutia vitendo vya utesaji katika mahabusu, unyanyasahi wa watu kutokana na dini zao, makabila au uungaji wao mkono wa makundi yenye silaha, mashambulizi dhidi ya wahudumu wa misaada ya kibinadamu na walinda amani na uingizaji wa watoto jeshini.