Ramadan Kareem waislamu wote Somalia:Keating

26 Mei 2017

[caption id="attachment_305627" align="alignleft" width="350"]hapanapaleramadhan

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Michael Keating , amewatakia kila la heri wato wote wa Somalia kwa kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Amesema Ramadhan ya kwama huu inafanyika wakati ambapo Wasomali milioni 6.7 wakiwemo maelfu ya wakimbizi wa ndani wanahitaji msaada wa kibinadamu kwa sababu ya ukame. Na kuongeza hilo linafanya juhudi za kuchagiza amani na kuboresha maisha ya watu nchini humo kuwa na maana zaidi na muhimu.

Keating amewataka Wasomali wote kwa niaba ya familia ya Umoja wa Mataifa Somalia kupokea salamu za kuwatakia Ramadhan Kareem.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter