Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi wa raia ni kitovu cha walinda amani-Lacroix

Ulinzi wa raia ni kitovu cha walinda amani-Lacroix

Kuelekea siku ya walinda amani duniani Mei 29, imeelezwa kuwa kazi ya kulinda raia ni jukumu kitovu cha walinda amani na licha ya ugumu wa kazi hiyo, ulinzi wa kundi hilo haukwepeki.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu operesheni za ulinzi wa amani Jean-Pierre Lacroix, amesema walinzi wa amani wanafanya kazi ngumu na hatarishi lakini akasema licha ya hayo.

(Sauti Lacroix)

‘‘Tutaendelea kufanya kila tuwezalo kusaidia raia ambao tuko kwa ajili ya kwasaidia na kuwalinda. Wakati mwingine ni ngumu sana, wakati mwingine hatuna rasilimali toshelevu za kufanya tutakalo. Lakini tunawahakikishia kuwa dhamiri na ahadi yetu ni kubwa sana hata pale tunapokabiliwa na changamoto inayofanya kazi hiyo kuwa ngumu.’’

Mwaka jana pekee walinda amani 90 wamepoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao.

Mwaka huu maudhui ya siku ya walinda amani duniani ni kuwekeza katika amani ulimwenguni kote, walinda wa Umoja wa Mataifa wamesema moja ya changamoto wanazokabiliana nazo ni tamaduni tofauti kule wanaokoenda kuhudumu.