Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ahadi za uwezeshaji SDGS ziwe halisi-Musiiwa

Ahadi za uwezeshaji SDGS ziwe halisi-Musiiwa

Mkutano wa ufadhili kwa maendeleo umeanza hii leo mjini New York Marekani, ikiwa ni ufuatiliaji wa mkutano uliopitisha ajenda ya ufadhili mjini Addis Ababa Ethiopia mwaka jana. Grace Kanieya na maelezo kamili.

(TAARIFA YA GRACE)

Awali katika mkutano huo , hadhira hii iliangalia ujumbe wa video kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Amina J. Mohamed ambaye amesema ushirikiano baina ya nchi wanachama ni muhimu katika kutekeleza ajenda ya uwezeshaji kwa maendeleo.

Kwa upande wake Rais wa baraza la uchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC, Fredrick Musiiwa, amesema utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu SDGs kupitia uwezeshaji utawezekana ikiwa washiriki wa mkutano watajadili kwa uwazi hatua zilizochukuliwa tangu mkutano wa Addis Ababa, na vikwazo vilivyopo.

Hivyo kiongozi huyo amesema.

(Sauti Musiiwa)

‘‘Ni jukumu letu la kimaadili  kutumia fursa hii kwa hekima, ili kuendeleza dunia katika kutekeleza SDGs na kuhakikisha ahadi zilizotolewa zinatimizwa.’’