Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mustkabali wa ndege wahamaohamao ndiyo mutskabali wetu :UNEP

Mustkabali wa ndege wahamaohamao ndiyo mutskabali wetu :UNEP

Leo ni siku ya kimataifa ya ndege wanaohamahama, Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP linasema ndege wanapohama safari zao ndefu hukabiliwa na vitisho kadhaa.

UNEP imesema mamilioni ya ndege huhama kutoka mabara hadi mabara mathalani kutoka barani Ulaya wanakozaliana hadi kusini mwa jangwa la Sahara kupata vyakula vyenye joto.

Ndege hukabiliwa na madhila kama vile kupoteza makazi ambako hutokana na hali ya ujangwa na mabadiliko katika kilimo na uwindaji. Kadhalika ndege wahamapo hupungua kwa kiwango kikubwa limesema shirika hilo la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira.

Borja Heredia ni mkuu wa kitengo cha ndege katika mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu viumbe vinavyohamahama.

(Sauti ya Heredia)

‘‘Lazima tuwalinde ndege kwa kuwa ni sehemu ya mazingira na sisi binadamu tunahusiana na afya ya mazingira. Kwa kuwalinda tunalinda mustakabali wetu pia.’’

UNEP imeonya kuwa ndege wahamao wako hatarini kutoweka ikitolea mfano wa ndege mashuhuri aina ya njiwa barani Ulaya ambao wametoweka kwa asilimia 90 tangu miaka ya 1970 na zaidi ya asilimia 90 nje ya Ulaya kati ya mwaka 1980 na 2014.