Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto zaidi ya milioni 1 wakimbia machafuko Sudan Kusini:UM

Watoto zaidi ya milioni 1 wakimbia machafuko Sudan Kusini:UM

Watoto wakimbizi ndio wamekuwa taswira ya hali ya dharura inayoendelea Sudan Kusini na kuuweka mustakhbali wa kizazi hicho njia panda.

Onyo hilo limetolewa Jumatatu na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR na la kuhudumia watoto UNICEF yakisema sasa zaidi ya watoto milioni moja wamekimbia machafuko yanayoendelea nchini humo.

Ukweli wa kuogofya ni kwamba karibu mtoto mmoja kati ya watano nchini Sudan kusini wamelazimika kukimbia makwao, ikidhihirisha hali mbaya ya vita hivyo amesema Leila Pakkala mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Mashirika hayo yanasema watoto ni asilimia 62 ya wakimbizi milioni 1.8 wa Sudan Kusini ambao wengi wamewasili Uganda, Kenya, Ethiopia na Sudan.

Ndani ya Sudan kusini kwenyenye watoto zaidi ya 1000 wameuawa au kujeruhiwa tangu kuanza vita 2013 na wngine milioni 1.14 ni wakimbizi wa ndani.