Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia bado inajikokota katika maafa ya magonjwa yanayozuilika– WHO

Dunia bado inajikokota katika maafa ya magonjwa yanayozuilika– WHO

Dunia bado inajikokota katika maafa kwa sababu ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kama ya moyo, saratani, matatizo ya kupumua na kisukari, ambayo hukatili maisha ya watu milioni 40 kila mkwaka.

Huo ni ujumbe uliotolewa na mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO, Dr Margaret Chan,anayeondoka baada ya kuliongoza shirika hilo kwa miaka 10.

Amesema magonjwa hayo yasiyo ya kuambukiza ni changamoto kubwa kwa dunia. Kitengo cha maradhi hayo kwenye ofisi ya WHO kinasimamiwa na Dr Doug Bettcher.

(SAUTI YA DR DOUG)

“Nadhani kuna kutokuelewa na kuna dhana potofu kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza na athari zake. Kuna fikra kwamba ndio kuna vifo vingi lakini huwezi kufanya lolote kuhusu hilo - hii ni dhana potofu. Baadhi ya haya magonjwa na hatari zake pia yana uhusiano na yale ya kuambukiza, kwa mfano kisukari, uvutaji sigara na lishe duni, yote ni sababu ya moja kwa moja ya kifua kikuu na ongezeko la vifo vya kifua kikuu.”