Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takwimu za satellite kutumika kufuatilia tija ya maji katika kilimo-FAO

Takwimu za satellite kutumika kufuatilia tija ya maji katika kilimo-FAO

Upimaji wa jinsi gani maji yanatumika katika kilimo hususani katika nchi zenye uhaba wa maji , sasa kufanyika kiteknolojia zaidi kwa msaada wa nyenzo mpya iliyoanzishwa na shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO.

Nyenzo hiyo mpya ya ukusanyaji takwimu kwa njia ya sateliti iitwayo WaPOR imeanza kutumika moja kwa moja Alhamisi baada ya kuzinduliwa kwenye hafla maalumu iliyofanyika makao makuu ya shirika hilo mjini Roma Italia.

Kwa mujibu wa FAO matumizi ya maji duniani ambayo mengi hutumika katika kilimo yamezidi kiwango cha ongezeko la idadi ya watu katika karne iliyopita na kupindukia matumizi endelevu. Jippe Hoogeveen ni afisa wa masuala ya ardhi na maji wa FAO anafafania nyenzo hii itakavyosaidia.

(SAUTI YA HOOGEVEEN)

"Nyenzo hiyo inaangalia maji kiasi gani yanatumika kwa kililo hususani katika umwagiliaji , hivyo maji kiasi gani yanahitajika kuzalisha chakula. Lakini tunapaswa kujua maji kiasi gani yanatokana na mali asili ili kuhakikisha hili linakuwa endelevu na kama kuna maji ya kutosha kuzalisha chakula"