Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zifahamu kazi na hamasa za wakunga kila siku

Zifahamu kazi na hamasa za wakunga kila siku

Benki ya Dunia na wadau wengine wanajizatiti katika kupunguza vifo vya mama mzazi na mtoto, pindi wanapojifungua. Nchini Nigeria, takriban milioni moja ya wakinamama na watoto hufariki dunia kila mwaka kutokana na magonjwa yanayozuilika. Ikiwa watapewa huduma za mara kwa mara za afya pale wanapobeba mimba hadi mtoto anapozaliwa, basi vifo hivyo vitapungua.

Nchini Nigeria, tunaangazia jinsi mhudumu mmoja anavyoshughulika kuwahudumia kundi hili. Ungana na Amina Hassan katika makala hii.