Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chad kuwa taifa la kwanza Afrika kutia saini mkataba wa kimataifa wa maji

Chad kuwa taifa la kwanza Afrika kutia saini mkataba wa kimataifa wa maji

Chad iko mbioni kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutia saini mkataba muhimu wa kimataifa kuhusu matumizi na upatikanaji wa maji imetanmgazwa Jumanne. Kwa mujibu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi kwa mataifa ya Ulaya UNECE inayosimamia utiaji saini mkataba huo, “Chad imesema bayana inataka kujiunga na mkataba huo haraka iwezekanavyo.”

Ziwa Chad ni chanzo cha nne cha maji kwa ukubwa barani Afrika lakini matawi yake husambaza maji hata nche ya mipaka ya nhi hiyo. Chad inasema na kwa sababu hiyo ni kwa manufaa ya taifa kutia saini mkataba huo wa maji ambao ambao unatoa jukwaa baina ya serikali mbalimbali kwa ushirikiano wa matumizi ya maji.