Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wenye usonji wanakosa haki za msingi za binadamu

Wenye usonji wanakosa haki za msingi za binadamu

Kwa kuzingatia haki za msingi za binadamu kwa watu wenye usonji, dunia inaishi kizani , kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya usonji.

Akizungumza Ijumaa katika tukio maalumu la kuadhimisha siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu usonji kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, profesa Simon Baron-Cohen mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa usonji kwenye chuo kikuu cha Cambridge Uingereza , amesema usonji ni ugonjwa wa maisha unaoathiri mishipa na kujitokeza kupitia ulemavu mbalimbali.

Akihojiwa na Umoja wa Mataifa Profesa Cohen ametaja baadhi ya changamoto zinazowakabili watu wenye usonji.

(SAUTI PROFESA COHEN)

Kuna baadhi ya ulemavu ambao uko bayana kwa mfano kama ni mtu usiyeoona, au ni mtu unayehitaji kiti mwendo, watu wengine wanauona ulemavu huo vyema, lakini usonji ni ulemavu usioonekana , kwa nje mtu anaonekana kawaida kama wengine lakini kwa ndani wanaweza kuwa wanataabika na mambo kama hamasa, ugumu wa kuchanganua mambo na wanaweza kuhitaji muda zaidi wanapofanya mambo ya kawaida kama kununua vitu. Na endapo hawatowezeshwa kwa ulemavu wao huo ni ubaguzi. Ni kama kumwambia mtu mwenye kiti mwendo kutumia ngazi.”

Siku ya uelimishaji kuhusu usonji uadhimishwa kila mwaka Aprili pili.