Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wa Guinea waliokwama Libya warejea nyumbani-IOM

Wahamiaji wa Guinea waliokwama Libya warejea nyumbani-IOM

Wahamiaji 98 raia wa Guinea wakiwemo wanaume 96 na wanawake wawili waliokuwa wamekwama Libya sasa wamerejea nyumbani Conakry kwa msaada wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Ndege ndogo iliyoandaliwa kwa uratibu wa serikali ya Libya na uongozi wa Guinea iliondoka uwanja wa ndege wa Mitiga tarehe 14 mwezi huu, huku shirika la IOM likifanya usaidi wa safari, uchunguzi wa afya na kutoa msaada mwingine kama mavazi na viatu.

Kwa bahati mbaya kutokana na mapigano mjini Tripoli wahamiaji 51 waliokuwa wakiishi maeneo ya mijini na waliokuwa wamepatiwa hifadhi ya malazi kwenye ubalozi wa Guinea usiku mmoja kabla ya safari wameshindwa kuondoka mjini Tripoli na kwa mujibu wa IOM watasaidia kurejea nyumbani Guniea kwa kutumia ndege za kibiashara. Kwa mwaka huu wa 2017 hadi sasa IOM, na serikali ya Libya imeshawasaidia wahamiaji 1261 kurejea makwao katika nchi mbalimbali wakiwemo watoto waliokuwa bila wazazi au walezi.