Skip to main content

Ujasiri wa wakazi wa Ziwa la bonde Chad unatia matumiani -Balozi Rycroft

Ujasiri wa wakazi wa Ziwa la bonde Chad unatia matumiani -Balozi Rycroft

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo hapa makao makuu jijini New York kuwasilisha ripoti yake kufuatia ziara yao ya bonde la Ziwa Chad, Amina Hassan nataarifa kamili.

(Taarifa ya Amina)

Akihutubi kikao hicho Balozi Matthew Rycroft wa Uingereza ambaye ni rais wa baraza hilo mwezi huu wa Machi na pia kiongozi wa msafara uliokwenda bonde la Ziwa Chad amesema kwamba madhila ya kusikitiisha na hali ya sintofahamu inayosababishwa na kundi la kigaidi la Boko Haram ni dhahiri miongoni mwa wakazi na ni matumaini yake kwamba ziara hiyo itakumbusha jamii ya kimatifa kuhusu madhilia wanayokumbana nayo wananchi.

Bwana Rycroft ameongeza kwamba kando na madhila wanayoyapitia, ushupavu na dhamira ya wenyeji wa Ziwa la bonde Chad kuleta amani na utulivu katika eneo hilo ni dhahiri kwani amekutana na wasichana wa Chibok walioshiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani jijini New York, Marekani ambao..

(Sauti ya Rycroft)

“Zaidi ya kuwa wahanga, zaidi ya kuwa waathirika sasa hivi ni wanaharakati wa kupiga kampeni ya kuelimisha wanawake na wasichana kuhusu umaskini. Licha ya machungu yote waliyopitia, licha ya kukumbwa kwenye sakata la Boko Haram, wameazimia kuangalia mustakhbali wao. Wameangazia kilicho mbele yao. Wamedhihirisha kuwa mustakhbali unawezekana pindi mapigano yatakapomalizika, silaha zitakaponyamazishwa na usalama utakapokoma kuwa nadharia na kuanza kuwa vitendo.”

Balozi Rycroft amesema mtazamo wao huo unadhihirisha kwamba suluhu la mzozo wa Chad ni la kisiasa na si kijeshi.